EXCLUSIVE : HAMISA MOBETO KUVISHWA PETE YA UCHUMBA TAREHE 2 YA MWEZI WA 8 NDANI ESCAPE 1.
Wanasema kimya kingi kina mshondo baada ya kudaiwa, hapo
mwanzo ilidaiwa kua Hamisa Mobeto alikua
akichepuka na Bwana Almas aka Dangote aka Diamond au Chibu kama mwenyewe
anavyopenda kujiita. Lakini baada ikaja kujulikana kua yalikua ni maneno ya
wabongo.
Habari za kuaminika Bongoclan ilizozipata ni kua kwa sasa
Mwanadada Hamisa kazama kabisa kwenye penzi zito la Seth De Jesus Giovan
almaarufu kama Bikira wa kisukuma. Mmoja wa mashostito wa wapenzi hao ambaye hakupenda
jina lake litajwe alisema kua Hamisa keshatambulishwa nyumbani kwao na Bikira
na kilichobaki ni tukio la kuvishana pete ndo lililobakia.
Team yetu iliamua kufatilia kama ni kuna ukweli kuhusiana na ishu ya kuvishana pete kwa
wapenzi hao na kugundua ni kweli kua watavishana pete tarehe 2 ya mwezi wa 8
ndani ya Escape 1 ambako pia ndani ya siku hiyo kutakua na Instagram Party.
Kupitia
akaunti yake bikira wa kisukuma alifunguka haya kuhusiana na tukio hilo
" Mungu anipe nini mie...Nimeokota Embe Dodo vhini ya Mpera..I cant
wait tarehe 2 pale ESCAPE 1.. Asante Mungu kwa kuileta INSTAGRAM maana
nisingempata huyu na kudolishia watu hapa... Nakupenda we mtoto kuliko
Ng'ombe anavyopenda majani,Nakuhusudu kuliko Mngoni anavyopenda
ngono,Nakuthamini kama Mchungaji anavyoithamini Biblia... I cant wait to
engage you pale jukwaani mbele ya halaiki maelfu TAREHE 2...Kama Chibu
kaweza kwanini mie nishindwe...Niko tayari kuwa bwege juu yako hamisa
wangu,Sitakuwa na wivu wala SitakuSPY kama mme wa yule dada nanii yule
mtangazaji,Msukuma nimezama kwako @hamisamobeto DONT MISS MY ENGAGEMENT
PARTY kwenye INSTAGRAM PARTY TAREHE 2...iam excited..Nikipigwa kibuti
ntalia balaa ntafunga akaunti wallah"
Pia inadaiwa kua Hamisa amewaalika mastar mbalimbali ambao
watahudhuria tukio hilo wakiwemo Diamond akisindikizwa na Wema, Adam Mchomvu, William Malecela, Jerry Slaa na
wengine kibao huku burudani ikitolewa na Skylight Band.
Kiingilio siku hiyo itakua ni elfu 10 tu huku mambo yakianza
mapema kuanzia saa1 ya usiku.
Unakaribishwa Kusoma habari za udaku na za siasa kila siku,
usikubali kupitwa, like page yetu ya swahilitz katika facebook na pia
usisahau kutufollow katika instagra @swahilitz vile vile katika twitter
@swahilitz1.
No comments