PICHA ZA AJALI YA GEORGE TYSON HUKO MOROGORO
"Gari alilopata nalo ajali Marehemu George Tyson saa kumi na mbili jioni May 30 2014 akitokea Dodoma - Dar es salaam. picha kutoka djchokamusic.com"
Picha hizi zilipigwa masaa manne kabla@jojityson hajapata ajali iliyo chukua maisha yake. "Marehemu Geogre Tyson pichani alikuwa yupo kijiji cha Chilonwa Chamwino Dodoma, kwenye utoaji wa madawati katika shule ya msingi Chaula iliyopo Dodoma. Baada ya kumaliza shughuli hii huku akiwa kama producer wa The Mboni Show mauti yalimkuta majira ya saa 12 jioni masaa 4 tu toka tuanze safari ya kurudi Dar es Salaam maeneo fulani hivi kama unataka kukaribia GAIRO mjini. Katika gari hilo walikuwa watu 8 ila yeye pekee ndio aliyepoteza maisha na wengine kupata majeraha mwilini pamoja na dereva wa gari hilo. Kwa sasa mwili wa marehemu umehifadhiwa hapa Morogoro katika hospital ya mkoa Morogoro, baadae asubuhi mwili utaanza safari ya kurudi Dar es Salaam." Msiba upo nyumbani kwa marehemu Bahari Beach.
No comments