USHAIRI: BY MORINGE JONASY MHAGAMA - NA WATAUA SANA
Redioni twasikia,kafa mwana jokofuni,
Wengine wamekimbia,na mapesa mfukoni,
Hao wamevumilia,mwisho warudi nyumbani,
Wataua kila siku,kilio chao kifike.
Memtoa kijijini,mrembo aje kupika,
Mwasema wa mkoani,kanga yake ya viraka,
Alalako ni jikoni,huyu naye anachoka,
Wataua kila siku,kilio chao kifike.
Mara akafue nguo,walipwa acha kudeka,
Mpaka za ndani nguo,amewahi kutapika,
Kipotea ufunguo,dadangu atachapika,
Wataua kila siku,kilio chao kifike.
Mshahara haupati,eti kavunja vikombe,
Waona hizi chapati,ungekula kwenu njombe,
Nasema pesa hupati,mara maziwa ukombe,
Wataua kila siku,kilio chao kifike.
Kaka akirudi shule,penzi lake alitaka,
Mama akiwa tandale,baba naye amtaka,
Dada akiwa mpole,na ziada atapata,
Wataua kila siku,kilio chao kifike.
Alea mtoto wako,wewe wamuita mbwa,
Mshahara uko kwako,wawa mbogo ukiombwa,
Hayupo mtoto wako,basi kamuua mbwa,
Wataua kila siku,kilio chao kifike...
USIMWITE BEKI TATU BASI,,,,,,,,,LOL.....
Wengine wamekimbia,na mapesa mfukoni,
Hao wamevumilia,mwisho warudi nyumbani,
Wataua kila siku,kilio chao kifike.
Memtoa kijijini,mrembo aje kupika,
Mwasema wa mkoani,kanga yake ya viraka,
Alalako ni jikoni,huyu naye anachoka,
Wataua kila siku,kilio chao kifike.
Mara akafue nguo,walipwa acha kudeka,
Mpaka za ndani nguo,amewahi kutapika,
Kipotea ufunguo,dadangu atachapika,
Wataua kila siku,kilio chao kifike.
Mshahara haupati,eti kavunja vikombe,
Waona hizi chapati,ungekula kwenu njombe,
Nasema pesa hupati,mara maziwa ukombe,
Wataua kila siku,kilio chao kifike.
Kaka akirudi shule,penzi lake alitaka,
Mama akiwa tandale,baba naye amtaka,
Dada akiwa mpole,na ziada atapata,
Wataua kila siku,kilio chao kifike.
Alea mtoto wako,wewe wamuita mbwa,
Mshahara uko kwako,wawa mbogo ukiombwa,
Hayupo mtoto wako,basi kamuua mbwa,
Wataua kila siku,kilio chao kifike...
USIMWITE BEKI TATU BASI,,,,,,,,,LOL.....
No comments