TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI JESHI LA POLISI TANZANIA MWAKA 2013
Jeshi la Polisi Tanzania linawaita kwenye usaili wahitimu walioorodheshwa hapa chini wa vyuo vya Elimu ya Juu na vya Ufundi Stadi.
Usaili
utafanyika kuanzia tarehe 11/11/2003 hadi tarehe 15/11/2013 saa mbili
asubuhi hadi saa kumi jioni kila siku kwa taaluma na maeneo yafuatayo;
- Fani za Menejimenti ya Rasilimali Watu, Utawala, Uchumi, Usimamizi wa Sheria na Utekelezaji(BaLe), Ualimu, Sosholojia, Saikolojia na Ushauri Nasihi, Sheria, Takwimu, Lugha, Uhusiano wa Kimataifa, Uandishi wa habari na Mawasiliano ya Umma, Maendeleo ya Jamii, Ukutubi na Utunzaji Kumbukumbu. Usaili wa fani hizi utafanyika katika chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es salaam(DPA) kilichopo kando kando ya barabara ya Kilwa Kurasini Dar es salaam .
- Fani ya Udereva ,Ufundi rangi za magari(spray and Painting /Panel Beating ), Ufundi wa matengenezo ya Magari Makubwa(Auto-Mechanics-Heavy Duty) na Ufundi wa Matengenezo ya Umeme wa Magari(Auto Elecrical ). Usaili wa fani hizi utafanyika Kikosi cha Polisi Ufundi kilichopo kando kando ya barabara ya Kilwa Kurasini Dar es salaam.
- Fani za Kompyuta. Usaili wao utafanyika nyuma ya kikosi cha Ufundi yaani TEHAMA KEKO chini.
- Fani ya Uhandisi Mitambo(Mechanical Engineering ). Usaili wao utafanyika Kikosi cha Polisi Anga kilichopo Uwanja wa Ndege JK Nyerere DSM.
- Waataalam wa masuala ya Afya/Wauguzi usaili wao utafanyika katika kikosi cha afya kilichopo kando kando ya barabara ya Kilwa Kurasini Dar es salaam.
- Orodha ya majina inapatikana pia katika Gazeti la habari Leo la tarehe 04/11/2013.
- (i)Mwombaji afike kwenyeakiwa na nakala halisi pamoja na kivuli cha vyeti vyote vya masomo/Taaluma [Academic Transcript (s)/Certificate(s)]yaani kidato cha nne, sita ,Chuo na cheti cha kuzaliwa. Hati ya kiapo cha kuzaliwa haitakubalika.
- (ii)Mwombaji aliyeitwa kwenye usaili atalipia gharamaupimaji afya shilingi elfu kumi(10,000), usafiri, chakula na malazi kwa muda wote wa zoezi la usaili.
(iii)Kwa kuwa muda ni mchache anaekuja kwa usaili ajiandae baada ya usaili atakaechaguliwa atapelekwa katika Chuo cha Taaluma ya Polisi Moshi siku nne baada ya usaili kwisha yaani tarehe 19/11/2013.
Orodha ni kama ifuatavyo;
No comments