MTAZAMO WA RAMA DEE KUHUSIANA NA ZITTO KABWE KUVULIWA MADARAKA KATIKA CHAMA CHA CHADEMA
Nimekaa na kutafakari nimegundua mambo mengi sana katika Nchi yangu
yenye Watu wenye matumaini....matatizo ya Chama cha Chadema ni sawa na
matatizo ya NCCR na CUF miaka iliyopita,Chama cha NCCR kilipewa
matumaini makubwa na Wananchi miaka ya tisini kikiongozwa na mwenyekiti
wake Mrema lakini zilifanyika mbinu kubwa za kukipunguza nguvu chama
hiki na si vingine kuwatumia watu ambao wapo ndani ya chama wenye nafasi
za juu...chama hiki walifanikiwa kukilipunguza nguvu na Wananchi
walipoteza imani kabisa, lakini inafikia sehemu Wananchi Haswa Wasanii
wenzangu tunatakiwa kusimama na Kutoziamini hizi propaganda pia inafikia
wakati wa kila mwananchi kufahamu mipango ya chama kama chama, Chadema
kumvua vyeo bwana Zitto ni sahihi kwa maslahi ya chama na katiba ya
chama hilo sio la kujadili, tujadili je hii njia ambayo inatumiwa na
Chama tawala kuvunja upinzani je tunaikabili vipi maaana inajirudia tu
kila ikifika uchaguzi mkuu wanatengeneza njia za kuvuruga
utaratibu, naomba tusiamini haya ambayo yapo mbele yetu tuamini kile
chama ambavyo kinasema nafikiri ndio njia rahisi ya ukombozi wa
elimu,afya nk,matatizo ya zitto haya tuhusu kwa sababu amevunja
utaratibu (kanuni) na chama kimethibitisha, Mbowe ni mwana chama na
kiongozi angekuwa anania mbaya na zitto basi hata hizo fulsa ambazo
amepata zitto asingezipata, mwanzo sikumfahamu ZITTO nilikifahamu Chama
na Chama kilimtambulisha, tukumbuke kila Chama kinaongozwa na katiba na
ndio maana ya Chama... Watanzania tumebakiza muda kidogo sana kupata
mabadiliko ni sisi kusimama na kuangalia wapi tunaelekea hizo ni siraha
za chama tawala kwenye kukimaliza chama na naaamini hawawezi MUNGU
BARIKI CHADEMA NA VIONGOZI WAKE yesu alisalitiwa kwenye Movment
zake,lakini aliendelea mbele mpaka walipoona wamemshindwa walimmaliza
ila ukweli ulibaki na upo mpala leo.... WATANZANIA TUSIMAME VIONGOZI
WANAFANYA AKILI ZETU KAMA "PLAY STATION TUSIMAME JAMANI HASWA VIJANA
WENZANGU NA WANAFUZI WA VYUO asanteni. USISHANGAE LEO KUONA ZITTO YUPO
CCM!!!!!
Source: Facebook (Rama Dee)
No comments