HUKU NDIKO WATANZANIA WENGI WANAKOISHIA BAADA YA KUACHA SHULE, EWE MZAZI BADILIKA NA MUANDAE MWANAO KUYAKABILI MAISHA
Katika historia ya watu wengi maarufu na wenye utajiri mkubwa duniani wengi wao hawakuweza kumaliza elimu yao na kuachia njiani na kujikita zaidi katika kuendeleza ugunduzi au shughuli mbalimbali walizozianzisha.
Kuna mifano hai mingi kama mmiliki wa facebook Mark Zuckerberg, Steve Jobs wa Apple Inc, Bill Gates wa Microsoft na wengine wengi, wote hao walikatisha masomo yao. Je sababu ni nini iliyowapelekea watu hao kuacha shule na kujikita zaidi katika shughuli zao binafsi? Je hali inakuwaje kwetu Afrika baadda ya kuchukua maamuzi magumu kama hayo? Tatizo kubwa ni tulivyoandaliwa na wazazi wetu katika kukabiliana na maisha, hatujaandaliwa kuzikuza talents tulizokuwa nazo(vipawa) na tumekuwa tegemezi zaidi katika kuajiliwa na si ajira binafsi ambazo zinaweza kuwa ndio mkombozi mkubwa wa maisha yetu. Mfano watoto wa mastaa wakubwa wa Hollywood Will Smith and Jada Pinkett , Willow na Jaden wamekuwa ni watoto waliokuzwa katika vipaji vyao mmoja cha muziki na mwingine cha uigizaji. Swali kubwa ni je. kwanini wazazi hao hawakuamua kuwapeleka shule wanao hao kama ilivyokwetu Afrika.
Tatizo kubwa ni kwamba wazazi wetu wamekuwa wapofu kwa kudhani kwamba mtu kuwa na elimu ya juu ndiyo kuwa na maisha mazuri, la hasha, kumkazania mwanao kushika madaftari na kutowakuza katika vipawa walivyonavyo ni sawa na kuwa na askari mwenye vyeo vimejaa mabega yote lakini hajui kushika silaha na kumkabili adui.
Ni wakati wa wazazi kubadilika na kuangalia dunia ya sasa inaendaje, waweze kuwaandaa watoto watakao weza kuikabili hali ya sasa na si kuwang'ang'aniza tu kwenda shule na mwisho wa siku wanarudi na matokeo mabaya na kuishia kuwa wazururaji wa mitaani wasio na muelekeo maalumu.
EWE MTANZANIA BADILIKA, MUWEZESHE MWANAO KUYAENDESHA MAISHA NA SI KUENDESHWA NA MAISHA.
Imeandaliwa na Kaozat (@kaozat1)
No comments