Habari mpya

REKODI ZA RONALDO BAADA YA "HAT TRICK YAKE" KUIPELEKA REAL MADRID NUSU FAINALI

                        Cristiano Ronaldo akishangilia moja ya magoli yake ya jana.

Usiku wa jana ulikua mzuri kwa mashabiki wa klabu ya Real Madrid baada ya kuepuka kipigo walichokipata nchini Ujerumapale walipofungwa magoli mawili kwa bila katika mechi ya mzunguko wa kwanza.
Real Madrid waliweza kurekebisha makosa yao na kujipatia magoli matatu kupitia kwa mchezaji wao tegemeo Cristiano Ronaldo.

                        Wachezaji wa Wolfsburg na Real Madrid wakiwania mpira.

   Magoli yaliyoitupa nje Wolfsburg yalifungwa na mreno huyo katika dakika za 16,17 na 77.

                           Zinedine Zidane kocha wa Real Madrid akishangilia hat trick ya mchezaji wake Cristiano Ronaldo

Nahodha na golikipa wa Wolfsburg Benaglio akimpa pole mchezaji mwenzake Luis Gustavo baada ya hat trick ya Ronaldo kukatisha ndoto yao ya kutinga nusu fainali.

Zifuatazo ni rekodi za Cristiano Ronaldo katika mashindano ya klabu bingwa ulaya.
                       MSIMU                                      MAGOLI
                   2013 - 2014                                            17
                   2015 - 2016                                            16
                   2015 - 2015                                            16   MSIMU HUU MPAKA SASA

Kutokana na rekodi hizi ronaldo anaweza kuvunja rekodi yake mweyewe ya kufunga magoli mengi kwani abdo ana mechi tatu amazo anatakiwa afunge magoli matatu ili avunje rekodi yake mwenyewe.
Rekodi zake zingine ni hizi
Mpaka sasa amefunga hat trick 5 katika mshindano ya klabu bingwa ulaya.
Amefunga jumla ya magoli 93 katika mshindano hayo.

No comments