Habari mpya

NDOA YANGU BADO IKO PALE PALE, AUNT EZEKIEL

Aunty Ezekiel msanii wa Bongo movies ambaye hivi karibuni alijifungua mtoto wa kike amesema kuwa licha ya kuzaa nje ya ndoa bado anaamini ndoa yake iko pale pale. Aunty amesema aliamua kuzaa na Moze Iyobo kwakuwa muda wa kuwa mama ulikuwa umefika.
" Niliamua kupata mtoto baada ya kuona wakati umefika na kwasababu siku zinaenda pamoja na umri inabidi maisha yaendelee. Ndoa yangu ipo kama ilivyokuwa mwanzo, haijavunjika, sijawahi kuongea kama nimezaa nje au ndani ya ndoa, mwisho wa siku ndoa yangu bado ipo lakini watu wajue baba yake ni moze. Source:Bongo5
Kumbuka Aunty alifunga ndoa na mtu mwingine hapo awali na anasema ndoa yake bado ipo ila tu ameamua kuzaa na Moze.

No comments